Preview
Description
Twende Dereva ni app ya kazi kwa madereva na wasafirishaji nchini Tanzania. Jisajili na chombo chako, uwe mtandaoni, na uanze kupokea maombi ya abiria na mizigo yaliyo karibu nawe. VYOMBO UNAVYOWEZA KUSAJILI Bodaboda, bajaji, gari, eGuta ya umeme, Town Ace, Kirikuu, Kenta, bowser ya maji safi, na malori ya kokoto na mchanga. Kazi hapa si ya abiria pekee. KUANZA 1. Pakua Twende Dereva na ujisajili na leseni yako na nyaraka za chombo. 2. Tunakuweka kwenye ramani ya wateja wanaokutafuta. 3. Pokea ombi, chukua abiria au mzigo, na ukamilishe safari. 4. Unalipwa kwa pesa taslimu au kwa simu, kutegemea mteja alivyochagua. UNAJUA KABLA HUJAKUBALI Kila ombi linakuonyesha umbali, mahali pa kuchukua na kiasi kabla hujakubali. Uamuzi ni wako. WEKA UMBALI WAKO MWENYEWE Chagua umbali wa juu unaokubali kwenda kumchukua mteja. Maombi ya mbali zaidi hayatakusumbua. MAPATO NA KUTOA PESA Ona mapato ya siku, wiki na mwezi ndani ya app, pamoja na kila safari na makato yake. Toa pesa zako kwenda kwenye simu yako wakati wowote. MIZIGO NA eGUTA Fanya delivery ndani ya mji na mizigo ya mkoa hadi mkoa. Kwa eGuta, waybill ya mzigo inapigwa picha na kuhifadhiwa ndani ya app, kwa hiyo wewe na mteja mnakuwa na kumbukumbu moja. MAJI SAFI Una bowser? Pokea maagizo ya maji safi ya kunywa kwenda nyumbani, ofisini na maeneo ya ujenzi. JUMUIYA YA MADEREVA Zungumza na madereva wenzako ndani ya app, ona nafasi yako kwenye jedwali la ushindani, na alika madereva wengine wajiunge kwa msimbo wako. NYARAKA ZAKO Pakia nyaraka zako ndani ya app na uone hali ya kila moja, ikiwa imethibitishwa au imeisha muda. Ukiongeza chombo kingine au kubadilisha, unafanya hapa hapa. MIJI Twende inapatikana Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Mwanza na Tanga, na miji mingine inakuja. Maelezo zaidi: www.twende.co.tz
What's New
Version 5.0.37 2026-11-04
App mpya ya Twende Dereva: muonekano mpya, ofa za safari zinafika haraka, mapato yanayoeleweka na kazi za eGuta. Technical Analysis
Package Overview Basic metadata
Bundle ID
com.twendetech.twendedereva Current Version 5.0.37
Minimum iOS 15.0
Package Size App Store Size
Package Metadata 0 / 1 version records
Detailed binary, privacy manifest, framework, and Info.plist results have not been indexed for this package yet. The verified App Store and archive metadata above remains available.
Known Version Records
0 version records with stored package metadata • 1 known version records
Stored metadata does not guarantee a package is currently available to download.
| Details | Version / IDs | Version date | Action |
|---|---|---|---|
| Not archived | App Store ID: 853635750 | Unknown | Request Version |